Sunday 12 April 2015

Kwa vazi hili lazima bibi harusi apendeze

Kutokana na imani zetu sote tunaamini kuwa mwanamke ni ua hivyo lazima apendeze kutimiza azima hii, hivyo linapokuja suala la harusi ibahitajika pia avae kile kitakachompendezesha .

Hiki si kitu kingine bali ni shela,ambao huwa maalumu katika sherehe hiyo kubwa kwa wanaotaka kuoana. Hakuna ubishi kuwa harusi  ni jambo la kheri kwa kila mtu bila kujali dini au kabila hivyo huhitaji maandalizi na mipangilio inayofaa ikiwemo suala zima la mavazi ambayo huwa maalumu kutokana umuhimu wa tukio lenyewe
Katika sherehe hii bwana haru na bi harusi huandaa nguo zuri zenye kupendeza kwa ajili ya kutimiza azima yao.
Ebu leo tuzungumzie vazi la bi harusi ambalo wengi tunalijua kwa jila la shela, hili ni gauni lililotengenezwa kwa ustadi mkubwa sana likizingatia mitindo ya kisasa ambayo itamfanya bi harusi kuepndeza na kuvutia machoni pa watu
Vazi hilo huwa refu kiasi cha kufunika mwili mzima wa bi harusi huku likiachia sehemu ya uso na mikono ambayo huwa kitambaa maalumu kilichopambabwa ilimradi mvaaji apendeze tayari kwa mumewe

No comments:

Post a Comment